Picha ya Atwoli na Aisha Jumwa Kwenye Kikao Yazua Mdahalo

Publish date: 2024-07-03

Picha ya Katibu Mkuu wa Miungano ya Vyama vya Wafanyakazi nchini COTU Francis Atwoli na Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa imezua mdahalo mtandaoni.

Picha hiyo ilipakiwa mtandaoni Julai 3 ambapo wawili hao wanaonekana wakifurahia baada ya kikao.

Kwenye picha hiyo pia ni mbunge wa Msambweni Feisal Bader na ajenda ya mkutano wao bado haijabainika.

Aisha ndiye alikuwa wa kwanza kupakia picha hiyo huku akiipa ujumbe maarufu unaohusishwa na Atwoli wa 'Alaar'.

Habari Nyingine: "Natrend na Sina Kitu": Jamaa Aliyesambaa Mtandaoni Aomba Usaidizi

Jumwa na Feisal ni baadhi ya wandani wa DP Ruto ambao wamekuwa wakipigia debe safari yake ya kuingia Ikulu.

Atwoli amekuwa mmoja wa wakosoaji wakuu wa DP Ruto na amekuwa akisisitiza hafai kuingia Ikulu 2022.

Jumwa amewahi kumrushia vijembe Atwoli baada ya kukosana kuhusu misimamo yao ya kisiasa.

Habari Nyingine: Jamaa Aliyepigwa Risasi Mara 8 Akikabiliana na Jangili Asema Alitaka Kumuokoa Rafiki

"Juzi niliskia ukisema Aisha Jumwa si size yako . . . wewe Atwoli tunajua size yako. Mashine yako twaijua wewe Atwoli, umezoea mshine ya Probox, V8 huwezani nayo," alimwambia Aisha.

Wanamtandao walisema kikao cha wawili hao ni ishara tosha kuwa Wakenya hawafai kukosa kwa ajili ya siasa.

"Ustadh Suleiman jibu ni kuwa usibebe chuki kwa siasa rafiki yangu. Utakuwa unajibeba ufala wewe mwenyewe," alisema Joseph Mulewa

Habari Nyingine: Laikipia: Jamaa Avamia Bunge la Kaunti Usiku, Aharibu Kompyuta na Kuhepa

Baadhi walisema huenda wawili hao walikuwa wamekutana na Atwoli kumshawishi kuingia kambi ya UDA.

Atwoli siku za hivi karibuni amekuwa akionekana mmoja wa vigogo washawishi haswa kuhusu siasa za 2022.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.

Tazama Video Kemkem za Kusisimua Kutoka hapa TUKO.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdkZoR3fpZmp6KbmJZ6uq2Mmquwp5yeeq%2BtjJqgrKCRYre2udaaZKSvlaPGpnnKoqKap12urrvBwGaknZmYlrmwesetpKU%3D